24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Gerrard: Nataka kupumzika na familia yangu

steven-gerrardLONDON, ENGLAND

BAADA ya kumaliza mkataba wake na klabu ya LA Galaxy, nyota wa zamani wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard, amedai kuwa anarudi nchini England kwa ajili ya kupumzika na familia yake kabla ya kurudi tena uwanjani.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, mwanzoni mwa wiki hii aliweka wazi kuwa hana mpango wa kutaka kustaafu soka kwa sasa japokuwa amemaliza mkataba wake na LA Galaxy, lakini bado ana nafasi ya kuendelea kucheza soka sehemu nyingine ila kwa sasa anataka kumpumzika na familia yake kwa muda.

Gerrard amesema kuwa tayari amepata ofa mbalimbali kwa ajili ya kuwa mchezaji na nyingine kuwa katika benchi la ufundi, lakini amesema kwa sasa anataka kupumzika na familia yake kutokana na kukaa mbali na familia kwa muda mrefu.

“Nimejifunza mambo mengi katika kuifundisha timu, naweza kuitumia nafasi hiyo kwa ajili ya kuzidi kusonga mbele na tayari nimepata ofa nyingi za kuwa kocha pamoja na kuwa mchezaji lakini naweka wazi kuwa kwa sasa natakiwa kupumzika.

“Kwa sasa natakiwa kurudi nyumbani nchini England kwa ajili ya mapumziko, lakini hii haimaanishi kuwa ndio mwisho wangu wa soka, bado nina mambo mengi ya kufanya katika soka na ninaamini muda mfupi ujao nitakuwa uwanjani katika klabu yoyote.

“Ndani ya wiki mbili hadi tatu chochote kinaweza kutokea, hivyo tusubiri kuona nini kitatokea,” alisema Gerrard.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, amekuwa akihusishwa kutaka kurudi katika klabu yake ya zamani ya Liverpool, baada ya kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp, kudai kuwa anatamani kufanya kazi na nyota huyo.

Hata hivyo, kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Celtic, ameweka wazi kuwa anataka kumsajili mchezaji huyo ndani ya kikosi chake na anaamini anaweza kufanikiwa kumnasa mchezaji huyo kutokana na mazungumzo ambayo yanaendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles