Fundi seremala adaiwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi

0
846

Twalib Salum -Mwanza

FUNDI seremala Daud Kabishi (40), amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa tuhuma mbili za kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi wa sekondari.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Ramsoney Salehe alimsomea mtuhumiwa hati ya mashtaka kwa maelezo ya awali.

Kwa kosa la kwanza la kubaka, Salehe alidai kuwa kwa nyakati tofauti toka Julai hadi Oktoba, mwaka huu, alikuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka15, kinyume na sheria ya watoto kifungu cha sheria ya jinai 130 (1) 2 (e) kama kilivyorejewa mwaka 2002.

Salehe akiwasomea shtaka la pili alidai kuwa kwa muda huo huo, alimpa ujauzito mwanafunzi wa sekondari kinyume na sheria ya elimu kifungu cha 60 (4) kifungu kidogo (4) sheria ya elimu sura ya 353 kama ilivyorejewa na sheria 2 ya mwaka 2016.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, Erick Marley baada ya mtuhumiwa kusomewa shtaka yote aliulizwa kama ni kweli tuhuma hizo, alikataa.

Kwa upande wa mashtaka umekamilisha ushahidi na utaleta mashahidi wanne na kielezo kimoja PF3.

Hakimu Marley alipanga kesi hiyo ianze kusikilizwa Januari 13 mwakani, mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana ya watu wawili kwa bondi ya sh milioni moja

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here