27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Tanesco yaanzisha makundi WhatsApp kutatua kero za wateja

Na MWANDISHI WETU

KATIKA kuhakikisha kuwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) linakuwa ka- ribu na kuweza kujua kero za wateja wake, limeanzisha makundi ya WhatsApp ili kujua namna ya kuwasaidia.

Ukitaka kutoa huduma iliyo bora ni vyema kuwa karibu na watu wako. Ndio maana Tanesco wametengeneza makundi kwenye WhatsApp ili kuweza kupata taarifa kuhusu matatizo ya umeme kutoka kwa wanaowahudumia.

Hatua hii ni agizo kutoka kwa wajumbe wa bodi ya Tanesco, ambapo makundi hayo yapo katika ngazi ya wilaya na mikoa Tanzania nzima.

Makundi hayo ni kulingana na aina ya wateja kwa maana ya wale wakubwa/wawekezaji wengine wakiwa wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

LENGO KUANZISHA MAKUNDI HAYO
Kwenye nchi yoyote, suala la upatikanaji wa nishati ya umeme ni muhimu kwa maendeleo. Tanesco wamekuwa lawamani kutokana na matatizo ya umeme, sasa makundi hao ndani ya WhatsApp yanalenga: Kutoa na kupokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wa kanda mbalimbali nchini na kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

KIONGOZI WA KIKUNDI

Ili mambo yaweze kusonga na kuleta matokeo chanya, ni lazima awepo kiongozi hivyo basi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco katika mtaa anaoishi ameunganishwa kuwa mteja wa Tanesco kwenye kundi la WhatsApp na wakati huo huo kuwa kiongozi.

Makundi hayo yatajumuisha wateja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tanesco lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati.

Akizungumzia utekelezaji wa agizo hilo, Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, anasema kuanzishwa kwa makundi ya WhatsApp kunalenga kutoa taarifa kwa wateja wao nchini kote.

Anasema hayo ni maagizo ya bodi ya shirika hilo ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

“Tunatambua nguvu ya WhatsApp katika kufikisha taarifa kwa jamii ndio maana tumeona hili na kuanzisha makundi hayo.

“Mameneja wa Tanesco kwa ngazi ya wilaya na mikoa wameanzisha makundi hayo kwa ajili ya kuwasiliana na wateja wao. Wapo viongozi wa ngazi mbalimbali wanaohakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatatuliwa kwa wakati,” anasema Muhaji.

Anasema hatua hiyo imeleta mafanikio makubwa kwani
hivi sasa wateja wa shirika hilo wanao uhakika wa kupata taarifa

ya kila kinachoendelea na wakati huo huo nao wanayo fursa
ya kuwasilisha changamoto zinazowakabili.

Katika kuhakikisha yanaleta tija zaidi, walichokifanya ni kuweka makundi kulingana na aina ya wateja, yapo yaliyounganisha wateja wakubwa ambapo miongoni mwao wamo wawekezaji.

“Kuna makundi ya wateja wa kati na na wa kawaida, kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

“Wamo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali ya mtaa, wakuu wa wilaya, wabunge na viongozi wengine ambao ni sehemu ya wadau muhimu katika kuhakikisha tunatatua changamoto za umeme,”anasema.

Anasema kupitia mfumo huo wamepata faraja kuona yamekuwa msaada mkubwa wa kufikisha taarifa zao kwa wateja huku akisisitiza kwa sasa wanahimiza wilaya zote za Tanesco kuhakikisha wanaanzisha makundi kwa wale ambao bado. Anasema kwa Dar es Salaam, wamekuwa wakipata taarifa kutoka wa wateja wao kwa haraka zaidi na watendaji wa shirika wanatafuta ufumbuzi kwa haraka.

0768 985 100

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles