Flaviana Matata afunguka kufanya kazi na Rihanna

0
843

Brighiter Masaki

MWANAMITINDO nyota nchini, Flaviana Matata, amesema watu wasishangae yeye kufanya kazi na mwanamuziki Rihanna kupitia bidhaa zake za urembo sababu amekuwa mwanamitindo wa Kimataifa.

Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Flaviana ambaye mwaka jana alionekana katika tangazo la bidhaa za urembo za Rihanna, alisema kazi yake ya mitindo imemkutanisha na mastaa kibao.

 “Rihanna ana kampuni mbili ya nguo na vipodozi, ninafanya naye kazi kwenye upande wa vipodozi, ni mchapakazi na mwenye upendo wa hali ya juu, ana ushirikiano na watu anaofanya nao kazi na anathamini mchango unaoleta kwenye kampuni yake,” alisema Flaviana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here