29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

YANGA WARUDI KWENYE MSTARI

Mwandishi Wetu, Singida

TIMU ya Yanga jana ilipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwaka huu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida United, mchezo uliochezwa  Uwanja wa Liti, Singida.

Ushindi huo, pia ni wa kwanza kwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Luc Eymael, ambaye alianza kibarua chake Jangwani kwa kupoteza mechi mbili mfululizo, dhidi ya Kagera Sugar ilipokubali kichapo cha mabao 3-1 kile cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ushindi huo umeipandisha Yanga hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza michezo 15 na kujikusanyia  pointi 28, ikishinda mara nane, sare na kuchapwa mara tatu.

Mabao ya Yanga yalifungwa na David Molinga dakika ya 12, Haruna Niyonzima dakika ya 58 na Ykipe Gnamien dakika ya 72, huku bao pekee la Singida United likifungwa na Six Mwasekagda dakika ya 83.

Yanga iliuanza mchezo kwa mashambulizi ya kasi.

Dakika ya 12, Molinga aliyeunganisha lifunga bao la uongozi la Yanga.

Dakika ya 19,  Deus Kaseke alilimwa kadi ya njano baada ya kuunawa mpira.

Kipa wa Singida United alifanya kazi nzuri dakika ya 26 kupangua kiki ya mpira wa adhabu iliyopigwa na Molinga.

Dakika ya 26, Molinga aliendelea kupoteza nafasi za kufunga kwani  wakati huu mpira wake wa kichwa ulitoka nje ya lango la Singida , akiunganisha kona ya Bernad Morrison.

Singida ilirejea mchezoni dakika ya 40 na kufanya  shambulizi, lakini kiki ya beki Mwinyi Haji lilipaa juu ya lango la Yanga.

Dakika ya 41, Molinga alishindwa kufunga bao akiwa yeye na mlinda mlango wa Singida, Owen Chaima baada ya kiki yake kupanguliwa.

Kipindi cha pili, Yanga ikizidisha kasi ya mashambulizi.

Dakika ya 48,  Haruna Niyonzima alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea madhambi Haruna Moshi ‘Boban’.

Singida United walifanya shambulizi lingine dakika ya 56 baada ya Mwinyi kupiga mpira wa krosi lakini mlinda mlango Metacha Mnata aliweza kuokoa hatari hiyo.

Niyonzima aliwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya 58,  baada ya kuunganisha krosi ya upande wa kushoto ya Morrison kwa shuti kali lililokwenda wavuni.

Mwamuzi Omary Mdoe, alimuonyesha kadi ya njano Papy Tshishimbi dakika ya 63 kwa kuonyesha mchezo usio wa kiungwana.

Dakika ya 64, Aron Lulambo alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea madhambi Morrison.

Dakika ya 66, Mdoe alimuonyesha kadi ya njano Boban, baada ya kumchezea madhambi Deus Kaseke.

Mshambuliaji Ykipe Gnamien, alikoleza shangwe za mashabiki wa Yanga dakika ya 72, baada ya kufunga bao la tatu akimalizia mpira uliotemwa na Chaima.

Mpira uliotemwa na Chaima ulitokana na kiki ya  Mapinduzi Balala.

Singida ilihamka dakika ya 83 na kusawazisha kupitia kwa  Mwasekaga, aiyeunganisha pasi ya Athuman Chuji.

Dakika 90 zilimalizika huku Yanga kuvuna pointi tatu, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, wageni Azam iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui, mchezo uliochezwa Uwanja wa Kambarage,  Shinyanga.

Bao pekee la Azam lilifungwa na mshambuliaji Shaban Chilunda dakika ya18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles