29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

FISI ALETA TAHARUKI HOSPITALI YA KAHAMA

Na PASCHAL MALULU-KAHAMA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mnyama mkali aina ya fisi ameonekana akirandaranda katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga na kusababisha taharuki kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa hospitalini hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo,  Dk. Lucas David, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa limetokea jana saa 12.30 alfajiri ambapo mnyama huyo alisababisha taharuki kubwa kwa wagonjwa wanaotibiwa hospitalini hapo.

David aliwaeleza waandishi wa habari kuwa taarifa ya mnyama huyo alipokea kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo aliyekuwa zamu kwamba mnyama aina ya fisi ameonekana hospitalini huku naye akitoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Anderson Msumba, ambaye alitoa taarifa kwa wataalamu wa misitu na mali asili.

Alisema baada ya hapo walipofika wataalamu hao aliungana nao ambapo fisi huyo walimkuta amelala nyuma ya ofisi ya mganga mfawidhi ndipo walipomuua kwa kumpiga risasi na kuondoka naye hadi ofisi za misitu na wanyama pori zilizopo nje kidogo ya mjini Kahama.

“Baada ya wataalamu kutoka idara ya wanyama pori kufika walifanikiwa kumuua akiwa amejificha nyuma ya jengo la mganga mfawidhi ambapo kuna tanki la maji lililokuwa linatumika hapo nyuma kuhifadhia maji na baada ya kumuua wataalamu hao walimchukua na kumpelea ofisi za mali asili kwa utaratibu mwingine,” alisema.

David aliongeza kuwa kwa taarifa walizopata kutoka kwa mganga wa zamu hakuna madhara yoyote yaliyosababishwa na mnyama huyo  licha ya kwamba wagonjwa waliingiwa na wasiwasi na kuongeza kuwa kwa sasa wagonjwa hali imekuwa shwari baada ya kuuawa mnyama huyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles