29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

ESMA: NIPO TAYARI KUWALEA WATOTO WA ZARI, HAMISA

Na KYALAA SEHEYE

KUFUATIA sakata la msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo, Hamisa Mobetto, dada wa mwanamuziki huyo, Esma Kandili ‘Esma Platnumz’, amesema yupo tayari kuwalea watoto wa kaka yake, Tiffah, Nillan na Dylan endapo mama zao watawasusa.

Tiffah na Nillan ni watoto wa Zarina Hassan ‘Zari the Boss Lady’ na Dylan ni wa Hamisa Mobetto.

Achonga na ShowBiz nyumbani kwao, Tandale Mhalitani, Esma, alisema kwa hali ilivyo sasa lolote linaweza kutokea na kama ikitokea watoto wakasuswa na mama zao – Zari na Hamisa basi yeye yuko tayari kuacha shughuli zake na kuwalea.

“Kama wifi zangu watatususia watoto basi wasijali mimi nitafanya kazi ya kuwalea kwani hii ni damu ya kaka yangu inanihusu kwa asilimia mia na ukizingatia mama yetu katuzaa wawili tu nitawalea kwa mapenzi yote kwa kuwa hao ndiyo ndugu zetu watakaotusitiri baadaye,” alisema Esma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles