27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Filamu ya EONII kuzinduliwa, Serikali kuboresha ‘vibanda umiza’

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha Sekta ya Filamu nchini inakua, Serikali imejipanga kuboresha vibanda vya kuonyeshea filamu mtaani (vibanda umiza) ili kuhakikisha kila mtu anafikiwa na kuangalia filamu za Kitanzania.

Akizungumza Juni 19, jijini Dar es Salaam na Waandishi wa Habari wakati wa kutangaza siku rasmi ya uzinduzi wa filamu ya EONII iliyoandaliwa na Azam Media kwa kushirikiana na Powerbrush, Katibu Mtendaji wa Mkuu Bodi ya Filamu, Dk. Kiango Kilonzo amesema kuwa Serikali inampango wa kuboresha vibanda hivyo ili kuendelea kukuza kiwanda cha filamu.

Amesema sekta ya filamu duniani imeendelea kukua na kupelekea pato litokanalo na kazi za filamu kufikia dola billioni 2.2.

“Bodi ya filamu ilibuni programu maalum ya kurejesha utamaduni wa kuangalia filamu kwenye kumbi za sinema lengo letu ni kuongeza pato kwa waandaji na wachezaji wa filamu,” amesema Dk. Kilonzo.

Naye Afisa Mwendeshaji Mkuu kutoka Azam Media, Yahya Mohamed amesema wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya sita kwa kusimamia Sanaa na kuweka mipàngo endelevu.

Amesema kutokana na hamasa, sera na kanuni madhubuti zilizowekwa na Serikali imesaidia timu ya uzalishaji kuwekeza ubunifu na umakini kwenye kuandaa filamu ya EONII.

“BODI ya filamu wamekuwa muhimili mkubwa katika hamasa, kuratibu njia sahihi za kuisukuma sanaa yetu ya filamu tunawashukuru sana na kipekee kabisa tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka chachu inayoipeka sanaa yetu ya filamu kimataifa,” amesema Mohamed.

Filamu ya EONII inatarajiwa kuzinduliwa Ijumaa Juni 23, 2023 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku wakitarajiwa viongozi mbalimbali kushiriki katika uzinduzi huo wa kiistoria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles