23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

IMO yawapiga msasa wadau wa bahari

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Shirika la Bahari Duniani (IMO) limetoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kutoka Taasisi zinazohusika na masuala ya bahari juu ya usalama na ulinzi wa Bandari na uwezeshaji salama wa vyombo vya majini.

Warsha hiyo iliyofanyika kwa muda wa siku tano, ilihitimishwa juzi jijini Dar es Salaam na na Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uje na Uchukuzi, Stella Katondo, akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara hiyo, Gabriel Mingile.

Akizungumza katika ufungaji wa warsha hiyo, Stella ambayo ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya IMO kwa kushirikiana na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), amesema mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kutoa elimu juu ya kuhusu utafutaji na uokoaji pindi inapotokea dharula majini.

“Lengo la mradi huu ni kuhakikisha maeneo ya bandari yanakuwa na ulinzi unaodhibitiwa na kuwa na usafirishaji salama katika maji na sisi Tanzania kama nchi Mwanachama wa Shirika la bahari, tume bahatika kupata bahati katika ukanda wa Magharibi wa bahari ya Hindi kwa Afrika Mashariki, kusini na visiwa vyake,” amesema Stella.

Aidha, amesema kama Wizara wamefurahia kuwepo kwa Warsha hiyo na kudai kuwa wao wameongea na IMO kupitia Shirika la TASAC kuongeza muda wa kuwepo kwa mafunzo hayo.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TASAC, Judith Kakongwe, ambaye pia alikuwa mshiriki katika warsha hiyo ya siku tano, amesema kuwa imewasaidia pia katika kuzijua sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles