24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

Filamu ya Bongo kuonyeshwa Netflix

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Huenda waigizaji wa filamu nchini Tanzania wakaonekana kwa mara ya kwanza katika jukwaa la Netflix ambalo huonesha filamu mbalimbali duniani.

Jambo hili linawezekanaje? Hii inawezekana baada ya mazungumzo kati ya waandaji wa filamu ya ‘Cops Enemy’ iliyoshirikisha waigizaji wa Tanzania na wanaoishi nje ya nchi na Netflix kukamilika.

Filamu hiyo imegharimu Sh. Milioni 200 imeongozwa na kuandikwa na muigizaji John Kay kutoka nchini Australia na Neema Ndepanya kutoka Tanzania.

Leo, Jumatatu Februari 4, Mtangazaji maarufu nchini Zamaradi Mketema ambaye ameshiriki kuandaa na kusimamia masuala yote yanayohusiana na filamu hiyo kwa hapa Tanzania amewataja wasanii walishiriki katika filamu hiyo kuwa ni Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Stanley Lusungu.

Waigizaji wengine na nchi wanazotoka kwenye mabano ni John Kay (Australia) na Van Vicker (Nigeria), filamu hiyo imechezwa maeneo mbalimbali ya Tanzania na Australia.

Amesema kwa muda mrefu waigizaji wa Tanzania wameshindwa kwenda kimataifa kwasababu hawakuwa na jukwaa la kuwafikisha huko lakini kwa filamu hiyo kuoneshwa katika Netflix itafungua mianya ya mafanikio na kutangaza Sanaa nje ya mipaka ya nchi.

“Filamu hi imekuja kuleta mapinduzi kwasababu kutengenezwa kwake tu imechukua miaka miwili tangu mwaka 2016-2018 na tunategemea kati ya Machi au Aprili mwaka huu tuizindue,” amesema Zamaradi.

Aidha Zamaradi amesema endapo filamu hii itafanikiwa kuoneshwa katika Netflix itakuwa ya pili kwa Africa baada ya Lion Heart ya muigizaji Genevieve Nnaji kutoka Nigeria kuoneshwa kupitia jukwaa hilo ambayo ndiyo ilikuwa ya kwanza.

Kwa upande wake muongozaji wa filamu hiyo Neema Ndepanya amesema katika filamu hiyo lugha iliyotumika ni kiswahili na wameamua kukitumia ili kutangaza lugha hiyo nje ya mipaka ya Tanzania.


- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles