29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

ETIHAD YAADHIMISHA MIAKA 10 YA HUDUMA INDIA

KERALA, INDIASHIRIKA la Ndege la Etihad katika kusherehekea miaka yake 10 ya kutoa huduma za usafiri wa anga katika Jimbo la Kusini mwa India, Kerala limeongeza huduma za ndege eneo hilo.


Etihad limezindua huduma ya safari za ndege mara nne kwa siku kati ya miji ya Kozhikode na Abu Dhab, lengo likiwa kuiunganisha miji mbalimbali duniani. 


Ongezeko la safari hizo kutalifanya shirika hilo kutoa huduma ya safari 63 kwa wiki kati ya Abu Dhab na Kerala ikifungua milango pia kwa miji ya Kochi na Kozhikode na mji kuu wa Kerala wa Thiruvananthapuram. 


Safari hizo ni sawa na asilimia 30 ya huduma za Shirika la Etihad kwenye majiji 11 nchini hapa.


Etihad lilikuwa shirika la kwanza la ndege duniani kuanzisha huduma za usafiri wa anga kwenye jiji la Kerala Mei 31, 2007.


Tangu hapo uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kerala  umekuwa sehemu muhimu ya usafirishaji ikiunganisha miji mbalimbali duniani na umeelezewa kuwa miongoni mwa kituo muhimu cha usafirishaji watalii nchini India. 

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles