24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 7, 2024

Contact us: [email protected]

ESAAMLG YACHAGUA TANZANIA KUWA MWENYEKITI VITA FEDHA HARAMU

Na FERDNANDA MBAMILA -DAR ES SALAAM

KATIKA jitihada zinazofanywa na Serikali za maendeleo katika kutekeleza mpango mkakati uliopangwa kwa mwaka wa bajeti 2017/18, malengo stahiki ni  kufanikisha ahadi kwa wananchi.

Mbali na mikutano mbalimbali inayofanywa na Serikali ndani na nje ya nchi katika kukuza na kuleta maendeleo  chanya ya kiuchumi nchini, imekuwa chachu kwa viongozi hao kuleta mwanga  kwa jamii kutokana na mwelekeo mzuri wa nchi kimaendeleo.

Baraza la Mawaziri wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika   ambao uliundwa kwa lengo la kusimamia na kudhibiti utakatishaji wa fedha  haramu, ulifanya kikao chake nchini hivi karibuni.

Umoja huo umeleta matumaini  makubwa baada ya mazungumzo yaliyofanywa na mawaziri wake hivi karibuni.

Mbali na  uwepo wa  mikutano  ya hapa na pale  inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kushirikiana na mashirika mbalimbali katika kujadili maendeleo  katika suala la udhibiti wa fedha.

Kuna umuhimu na jitihada kufanyika kulinda na kuthamini fedha ya nchi kwa kuweka udhibiti na ulinzi na usalama dhidi ya fedha haramu, ambazo zinatengenezwa na kuingizwa nchini  kwa manufaa ya watu fulani wachache.

Hapo awali kulikuwa hakuna chombo maalumu, taasisi au umoja wowote ambao kwa namna moja au nyingine ungeweza kusimamia na kudhibiti fedha haramu kuingia na kutoka nchini.

Kwa sasa  kumekuwa na udhibiti na ulinzi  wa hali  ya  juu katika mipaka na sehemu mbalimbali  ambazo kuna mwingiliano na mikusanyiko mikubwa ya watu.

Tanzania  ilikuwa mwenyeji wa mkutano  wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa nchi za Mashariki  mwa Kusini  mwa Afrika  wa Kudhibiti Utakasishaji  wa Fedha Haramu (The Eastern and Southen Anti Money Laundering Group,  ESAAMLG).

Mkutano huo ulifanyika Zanzibar Septemba 8, mwaka huu katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar, ulikuwa na lengo la kujuzana na  kuelezana  hali halisi ya mipaka ya nchi wanachama.

Mkutano huo ulitanguliwa na mkutano wa maofisa waandamizi kutoka nchi wanachama wa umoja huo uliofanyika Septemba 2, mwaka huu.

Rekodi zinaonesha kuwa nchi wanachama ni Angola, Botswana, Comoros, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius,  Msumbiji, Namibia na Afrika Kusini.

Nchi nyingine ni Rwanda, Swaziland, Seychelles, Tanzania, Uganda, Zambia  na  Zimbabwe.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulifunguliwa na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, kwa niaba ya  Dk. Magufuli.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Mawaziri wote wa nchi wanachama  wa Umoja wa ESAAMLG.

Mbali na hayo, mkutano huo ulijadili mambo mbalimbali  ikiwa ni pamoja na  hatua madhubuti iliyofikiwa na nchi wanachama katika kuimarisha mfumo wa Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi.

Aidha, mkutano huo walipitisha mikakati mbalimbali ambayo itasaidia nchi wanachama kuimarisha mipaka ya nchi zao.

Katika muundo wa kiutendaji wa Umoja wa ESAAMLG, unajumuisha Baraza la Mawaziri ESAAMLG (Council of Ministers) na sekretarieti ya ESAAMLG.

Baraza la Mawaziri  ndicho  chombo cha maamuzi cha mwisho katika umoja na hufanya mikutano ya mwaka  kati  ya mwezi  Agosti  na Septemba.

Katika mkutano uliofanyika mwaka huu, Tanzania  ilikabidhiwa uenyeji wa Umoja wa ESAAMLG kwa kipindi cha mwaka mmoja, ambapo Waziri wa  Fedha, Dk. Philip Mpango, alikabidhiwa  kijiti cha Urais wa Baraza la Mawaziri la Umoja wa ESAAMLG (President of Council) naye Onesmo Makombe, ambaye  kwa sasa ni Kamishna wa  kitengo cha  kudhibiti fedha haramu,  huyo ndiye aliyekabidhiwa uwenyekiti wa Mikutano ya Maofisa Waandamizi (Chairman of the Task Force Senior  Officials).

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles