23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

ELIMU KIKWAZO WAGONGWA KUPATA HAKI

VERONICA ROMWALD NA ABDALLAH NG’ANZI (Tudarco)

– DAR ES SALAAM

UELEWA mdogo wa jamii kuhusu sheria ya matibabu unachangia wagonjwa wengi kukosa haki zao za msingi hasa wanapokuwa wamepatiwa matibabu ambayo si sahihi.

Hayo yalielezwa jana na Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania, Maulid Kikondo alipozungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu jana.

Alisema kutokana na wagonjwa wengi kutoifahamu sheria hiyo wamejikuta wakiishia kulalamika bila kuchukua hatua za kisheria dhidi ya daktari pale wanapopatiwa  matibabu yasiyo sahihi.

“Zamani huduma za afya zilikuwa zikitolewa kwa kiwango kikubwa katika vituo vya afya vya serikali lakini leo hii kuna vituo vya serikali na vipo vya binafsi, huduma za matibabu  zimekuwa biashara, wakati mwingine wagonjwa wamejikuta wakifanyiwa vipimo vingi ambavyo vingine hata havistahili kwa wakati huo,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, wataalamu wa sheria walipendekeza kutungwa kwa sheria hiyo ili kulinda haki za mgonjwa.

“Sheria hiyo inaitwa Medical Negligence ndani yake kuna kipengele cha ‘Medical Legal’ ambacho chenyewe kinalinda haki za mgonjwa na inapendekeza iwapo atapatiwa matibabu yasiyo sahihi inamwajibisha daktari aliyemuhudumia,” alisema.

Alisema sheria hiyo ilitungwa mahususi kwa ajili ya kuimarisha uwajibikaji katika utoaji wa huduma za matibabu duniani.

“Mataifa mengi yanaitumia sheria hii na hapa nchini madaktari wote wanaifahamu lakini jamii bado ina uwelewa mdogo matokeo yake unakuta mgonjwa anapatiwa huduma isiyokuwa sahihi, kwa mfano amepatiwa matibabu ambayo yamemsababishia ulemavu kimsingi ana haki ya kushtaki mahakamani.

“Mahakama itakaa na kusikiliza kesi kwa kutumia sheria hii na ikiwa daktari atapatikana na hatia kwamba alifanya uzembe mgonjwa anakuwa na haki ya kudai kulipwa fidia,” alisema.

Kikondo alisema pamoja na kulinda haki za mgonjwa sheria hiyo pia hulinda haki ya daktari hasa anapokuwa anatoa huduma ya dharura kuokoa maisha ya mgonjwa.

“Kwa kawaida mgonjwa kabla ya kupatiwa matibabu ni lazima iwepo idhini baina yake na daktari lakini wakati mwingine hutokea mgonjwa akahitaji huduma ya haraka kwa mfano mtu amepata ajali pale huwa hakuna haja ya kusubiri idhini kutoka kwake au ndugu zake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles