28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ateta Ikulu na Waziri wa Japan

Na Mwandishi Wetu

-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Ichiro Aisawa Ikulu, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, waziri huyo wa Japan alimpongeza Rais Magufuli kwa uongozi mzuri, kupambana na rushwa na msukumo mkubwa anaoutoa katika maendeleo, juhudi ambazo zinasaidia kuimarisha uchumi na kuboresha huduma za kijamii.

Waziri Ichiro alitembelea baadhi ya miradi inayojengwa hapa nchini na kampuni za Japan ukiwamo mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover) wa Tazara na mradi wa kuzalishaji umeme kwa gesi wa Kinyerezi II na alimuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hizo zitafanya kazi nzuri na zitakamilisha kazi kama ilivyopangwa.

Alisema baada ya kuona changamoto ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam, amebaini kuwa nchi yake bado inahitaji kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha miundombinu ya jiji hilo na aliahidi kufikisha ujumbe huo kwa Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimshukuru Waziri Ichiro kwa kuja nchini na amemuhakikishia kuwa Tanzania inatambua mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo.

“Naomba unifikishie ujumbe kwa Waziri Mkuu Shinzo Abe kuwa Tanzania inamshukuru kwa ushirikiano huu mkubwa, tunamkaribisha sana Tanzania na kwa kuwa Serikali yetu imehamia Dodoma, tutafurahi sana kama Japan itaweka alama ya urafiki wetu kwa kutujengea barabara za Dodoma mjini, iwe ni flyover au kilometa 20 za barabara, sawa tu,” alisema Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles