28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Ekari 535 za mirungi zateketezwa Kilimanjaro

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Jumla ya ekari 535 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa katika oparesheni maalum ya ‘Tokomeza Mirungi’, iliyoanzia kutekelezwa ndani ya vijiji vya Rikweni, Heikondi, Tae na Mahande, wIlayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro.

Oparesheni hiyo intekelezwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ikishirikiana kwa karibu na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama likiwamo Jeshi la Polisi Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema katika oparesheni hiyo jumla ya watuhumiwa saba wamekamatwa.

Amesema mirungi ni mojawapo ya dawa za kulevya zilizokatazwa nchini kwani ina athari nyingi kwa binadamu, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiafya.

“Inasababisha saratani ya koo, utumbo na uraibu, mtindio wa ubongo, kiuchumi inasababisha nchi inakosa mapato kwa sababu wengi wanaolima mirungi Kata hii na eneo hili la Same hawaingizii mapato yoyote Serikali.

“Lakini pia tunahakikisha kwamba kwenye mikataba ya kimataifa ambayo tuliingia mwaka 1961, 1971 na 1986 inatutaka nchi yoyote iliyoingia ile mikataba ihakikishe inafanya oparesheni katika maeneo yake yote,” amesema Kamishina Lyimo.

Amesema ili kuhakikisha kwamba inatokomeza kabisa suala la dawa za kulevya katika nchi husika, pia lazima ioneshe juhudi inazofanya katika kutokomeza dawa za kulevya kwa wananchi na jamii nzima.

Amesema dunia iweze kuona kuwa kazi inayofanywa na nchi husika katika kutokomeza dawa za kulevya.

Kamishna Lyimo amesema kwa sababu hiyo ndiyo maana DCEA imepiga kambi mkoani humo kwa ajili ya oparesheni hiyo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola.

Amesema hekari hizo zimeteketezwa kwa muda wa siku nane kuanzia Julai 2 hadi 9, mwaka huu.

“Kwa hiyo niwashukuru wote ambao tunashirikiana nao katika oparesheni hii, tuwaombe wananchi wote kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan, viongozi wote wa Serikali, mkoa, wilaya, vijiji na Kata.

“Tushirikiane kuhakikisha tunatokomeza dawa za kulevya, mashamba yote hususan katika eneo hili la Wilaya ya Same, lakini pia tuhakikishe kwamba tunaijengea Serikali uwezo wa kuweza kufanya shughuli zake,” amesema.

Amesisituza wamekuja eneo hili wameona Serikali ilivyojenga miundombinu, maji yapo ya kutosha, imeweka miundombinu ya umeme, barabara inatumia kodi za watu wengine kuja kuweka miundombinu huku.

Amesema Wakati huku wao wanalima mirungi na hawaingizii Serikali Pato lolote na madhara yanayopatikana kwa wananchi, kwa jamii na mtu mmoja mmoja ni mzigo kwa Serikali pia.

Ameongeza wameona hekari nyingi imewashangaza, hatukutegemea kuna hekari kubwa kiasi hicho hadi wanachukua vikosi vya Jeshi JKT kuja kufanya oparesheni hii na kununua mashine za kuteketeza

Aidha ameihasa jamii yote kwa ujumla, viongozi wa dini, kimila, Serikali kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji, kata na mkoa wote kushirikiana na DCEA kutokomeza biashara ya dawa za kulevya.

“Tanzania inawezekana kuwa salama kwa kutokuwa na dawa za kulevya, Sheria pia imetutaka kwamba ukishakamata shamba limelima dawa za kulevya inaruhusu kutaifisha shamba hilo,.

“Tuiombe jamii tukishaanza kutaifisha mashamba yao, watakosa hata maeneo ya kulima, kuanzia sasa tutaanza kuitekeleza, tukikuta shamba lako limelima bangi, mirungi tunataifisha,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles