29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

TANTRADE kufanya tathmini ya maoneysho ya Sabasaba

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) inatarajia kufanya tathimini ya maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Julai 13, mwaka huu kueleza fursa mbalimbali zilizopatikana.

Hayo yamebainishwa Julai 10, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis kwenye maonesho hayo ikiwa ni siku maalumu ya wafanyabiashara wa India lakini siku maalumu kwa jimbo la Haryana, ambapo amesema mwaka huu wameshuhudia ubunifu wa siku maalumu wa nchi mbalimbali.

Amesema kwa nini wamekuja na siku hizo maalumu kwa sababu wameangalia fursa zilizopo katika maeneo hayo kwasababu wadau wengi wanashirikiana nao.

“Asilimia 50 tumewezeza kufanikiwa ambacho tumejipangia kuwanacho kwenye maonesho ya 47 sabasaba, Watanzania wajiandaea kwa maonesho ya 48 na kuhakikisha wanakuja na vitu vingine zaidi na maandalizi tayari tumeanza,” amesema Latifa.

Amesema walipanga kuwa na siku maalumu ya nchi tatu ambazo ni Iran, China na India hatimae wamekamilisha.

Ameelezea kuwa Haryana ni jimbo moja kati ya majimbo linaongoza katika uchumi nchini India katika sekta ya kilimo, madini na viwanda hivyo Watanzania kujua fursa zilizopo kwenye serikali ya jimbo hilo ni muhimu kwa ajili ya ushirikiano.

Aidha, amesema katika siku hiyo maalumu waliambatana na msafara uliojumlisha zaidi ya wadau 50 na viongozi wa jimbo hilo wameshiriki, lengo kuwaonyesha Watanzania fursa zilizopo. .

Amesema wana mikataba mikubwa na ya manufaa baina ya Tanzania na India na uhakika serikali ya jimbo hilo ipo hapa kuhakikisha kila mmoja anaondoka na fursa mbalimbali.

Julai 12, mwaka huu wanatarajia kuhitimisha siku maalum za maonesho ya 47 ambao watakuwa na siku maalumu Zanzibar kutakuwa na “Promotion” ya uchumi wa bluu na bidhaa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa Bodi TanTrade, Profesa Ulingeta Mbamba amesema wameweza kusikia mambo mengi ambayo India wanaweza kuleta nchini na vitu ambavyo Tanzania itapeleka nchini humo.

Amesema nia inaendeshwa na biashara ni muhimu katika fursa zote kwenye biashara na kwa kiasi gani Tanzania inaweza kutumia.

“Pia Taifa la India linaweza kuendeleza maendeleo ya nchi zotee mbili tumekuwa tunaagiza vitu vingi toka India mfano madawa ,vifaa vya ujenzi, mashine na vitu vingine,” amesema Profesa Mbamba.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Serikali ya Haryana, Dk. Raja Vundru amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali.

“Nchi hizi mbili zinauhusiano mzuri katika biashara, kuna bidhaa za Tanzania zinapatikana India kama parachichi ngano na mengine na bidhaa za India zinapatikana Tanzania huo ni uhusiano mzuri,”amesema Dk .Vundru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles