Dulvan kurudisha shukrani kwa mashabiki zake

0
610

BEATRICE KAIZA

Katika kurudisha fadhila kwa mashabiki zake, msanii anayekimbiza kwenye tasnia ya uchechi nchini, Abdallah Sultan ‘Dulvan’ anakuja na shindano lako alilolipa jina la asante Fans Dula Van.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mei 19, amesema vigezo vya kushiriki kwenye shindano hilo ni kumfwatilia kwenye mitandao yake ya kijamii kwa njia ya kucomment na kuwatag watu wa tano kwenye picha ambazo atakuwa anatuma kwenye mtandao wake wa Instagram na kupata mshindi kwa kila wiki mmoja.

“Asante Fans  Dulla Van ni shindano ambalo litakuwa linafanyika kwa njia ya simu na nimeamua kufanya hivyo kwa lengo la kurudisha shukrani kwa mashabiki zake kwa mafanikio ambayo nimepata kutoka kwa kwao,” amesema Dulla Van.

Ameongezea kuwa kwa wiki hii mshindi atapata kiasi cha Shilingi laki 5 kwa watu wa tano na kwamba shindano hilo halichagui ni kwa watu wote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here