Dudubaya afutiwa usajili Basata

0
1345

Na Asha Bani-Dar es Salaam

Msaani wa Bongo fleva Godfrey Tumaini aka Dudubaya leo amefutiwa usajili na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), na kutotakiwa kujishughulisha na shughuli zozote za sanaa hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kutika kwa katibu Mkuu wa BASATA Godfrey Mngereza, amesema kwa kuzingatia sekta ya sanaa na kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 1984 ikisomwa kwa pamoja na marekebisho yote ya mwaka 2019 kupitia kifungu 4(3) sura 204 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Mivhezo ameaigiza kuchukua hatua dhidi ya msanii huyo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 4(2) sura ya 204 kinachotoa mamlaka kwa Baraza kufanya jambo lolote kwa maendeleo ya sekta ya sanaa kwa ujumla imefuta usajili wake sambamba na cheti chake cha usajili chenye namba BST 2184,

“Pia kimefutwa na kuanzia sasa hatoruhusiwa kujihusisha ba shughuli zozote za sanaa hapa nchini wala kupata nafuu yeyote kutoka baraza kama msanii, ” aliongeza Mngereza.

Alisema uamuzi huo unatokana na kitendo cha msanii huyo kutumia lugha za matusi kwa wadau wa sanaa kupitia akaunti yake ya Instragram huku akutambua kuwa yeye ni msanii aliyesajiliwa na Baraza hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here