DC Ilala apiga marufuku mikusanyiko kwenye baa; ‘nunua ukanywee nyumbani’

0
962

Asha Bani, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amepiga marufuku mikusanyiko kwenye baa zote wilayani humo kuanzia leo Ijumaa Aprili 17 ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.  

Amewataka waendesha baa hizo, kuhakikisha wanauza vinywaji hivyo lakini lakini mnunuzi akanywee nyumbani na kwamba atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua.

“Ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo haya kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mwendeshaji wa baa na mtu yeyote atakayeonekana kwenye eneo la baa akiendelea kunywa,” amesema Mjema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here