26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Dortmund yaitandika Manchester United 4-1

 

lingard

SHANGHAI CHINA,

TIMU ya Manchester United imejikuta ikipokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa  Borussia Dortmund katika mchezo uliochezwa jana katika jiji la Shanghai nchini  China katika michezo ya michuano ya Kombe la Ubingwa wa  Kimataifa (ICC).

Kabla ya mchezo huo Mourinho alidaiwa kusema kwamba kikosi chake kilitakiwa kuwa makini dhidi ya wapinzania wao hao.

Mchezaji mpya wa timu hiyo  Henrikh Mkhitaryan alifunga bao la kufutia machozi la timu hiyo dakika ya 59.

Mbao ya Dortimund yalifungwa na Gonzalo Castro dakika ya 19 na 86 huku Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 36 na  Ousmane Dembele dakika ya 58.

Miongoni mwa timu kubwa zinatarajia kushiriki michuano hiyo Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint German (PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles