26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Laporta: Messi hatendewi haki Barcelona

messi

BARCELONA, HISPANIA

RAIS wa zamani wa klabu ya Barcelona Joan Laporta, ameikosoa bodi ya klabu hiyo kwa kushindwa kukitunza kipaji cha mshambuliaji Lionel Messi uwanjani.

Laporta aliwahi kuwa rais wa klabu hiyo mwaka 2003 na kufanikiwa  kusimamia mafanikio ya klabu hiyo kabla ya kumaliza muda wake miaka saba iliyopita.

Mgogoro wa  katikati ya msimu wa  2014/15 katika klabu hiyo usababisha kuitishwa kwa uchaguzi ambapo Laporta alisimama kugombea lakini alishindwa kutamba mbele ya Josep Maria Bartomeu.

Akiwa katika mahojiano na redio moja maarufu jijini Catalunya, Laporta alisema kwamba hafurahishwi kabisa na namna ambavyo Bartomeu anavyoendesha klabu hiyo.

Laporta alisisitiza kwamba Bartomeu alitakiwa kujua namna ya kuishi katika kipaji cha Messi.

“Klabu hadi sasa haijafahamu namna ya kuishi na kipaji cha Messi, ni mchezaji bora wa kihistoria pia mchezaji bora duniani.

“Bartomeu amefeli kutimiza moja ya ahadi yake wakati akisaini dili la udhamini mpya na Qatar Airways” alisema Laporta.

Laporta aliendelea kumtupia lawama mpinzani wake huyo kwa kudai kwamba ni mwongo.

“Alitudanganya kwenye kampeni kwamba angeweza kupokea dili zenye thamani ya euro milioni 60, lakini hadi sasa hakuna kitu kama hicho,” alihoji Laporta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles