Dogo Rama, Kupaza waanzisha bendi yao

dogo rama...NA MWALI IBRAHIM

WANAMUZIKI waliokuwa wakiunda bendi ya Double M Plus, Saleh Kupaza na Ramadhani Athumani ‘Dogo Rama’, wameanzisha bendi yao binafsi iitwayo Ivory baada ya kutofautiana na bendi ya Double M na Twanga Pepeta.

Mmoja ya wanamuziki wanaounda bendi hiyo, Rama Pentagon ‘Chewa’, alisema bendi hiyo mpya imeanza mazoezi jana katika kambi yake iliyopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Pentagon aliwataja baadhi ya wanamuziki waliowang’oa kutoka bendi ya Double M Plus ya ‘Kocha wa dunia’, Muumini Mwinjuma ni mpiga besi, Jojo Jumanne, mpiga rhythm, Rashidi Sumuni, Sele Kadansi, Sisila, Sharon na Amina Juma.

Wanamuziki wengine waliowachukua kutoka bendi ya The African Stars Twanga Pepeta ni mpiga solo mahiri, Ally Akida ‘Tetenasi ya Giniva’.

Pendagone aliongeza kwamba watakuwa wakipiga muziki wa tofauti sana kutokana na kuwa na kikosi chenye uwezo mkubwa katika muziki.

“Tutakuwa tukipiga muziki wa dansi tofauti na uliozoeleka lakini pia tukijikita kupiga kopi mbalimbali ili kupata soko la ndani na la kimataifa ambapo tayari tumeshapata mialiko wikiendi hii,” alieleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here