32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Dodoma yaongeza uwezo wa kujitegemea

Na SARAH MOSES -DODOMA


HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeongeza uwezo wake wa kujitegemea kwa kutumia mapato ya ndani kutoka asilimia tisa za awali hadi kufikia 34 kwa mujibu wa taarifa ya hesabu za fedha kwa mwaka ulioishia Juni 2018.

Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa jana na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha.

Alisema hadi sasa jumla ya Sh bilioni 14  zimeshakusanywa na lengo lake ni kukusanya jumla ya Sh bilioni 67 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019.

“Halmashauri ya Jiji la Dodoma ndiyo inayoongoza kwa kujitegemea ikifuatiwa na Manispaa ya Ilala iliyopo Dar es Salaam.

“Endapo halmashauri yetu itajitegemea yenyewe bila kupokea fedha kutoka Serikali kuu, ina uwezo wa kujiendesha kwa muda wa miezi mitano,” alisema.

Kuhusu ukusanyaji mapato kupitia vyanzo vya ndani, alisema hali ya makusanyo si mbaya kwa sababu wamekusanya kiasi cha Sh bilioni 14 sawa na asilimia 22 kwa Julai hadi Septemba, mwaka huu wa fedha.

“Mfumo wa ukusanyaji mapato unaojulikana kama Local Government Revenue Collection Information System (LGRCIS) umechangia kutokufikia malengo yetu kwa sababu tulipanga kukusanya mapato kwa asilimia 25,” alisema.

Kwa upande wao, wajumbe wa mkutano huo wakiongozwa na Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe, walipongeza halmashauri hiyo kupiga hatua katika makusanyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles