31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Dk.Tiboroha bosi Azam FC

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Dk. Jonas Tiboroha, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Soka wa Azam FC cheo ambacho ni kipya katika klabu hiyo.

Akizungumza wakati wa kumtambulisha Dk. Tiboroha, leo Jumatatu Agosti 16, jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdulkarim Amin’Popat’, amesema atakuwa akisimamia maendeleo yote ya soka katika klabu hiyo.

“Kwa uzoefu wake na kuwa kwenye mpira kwa miaka mingi, tunategemea atatusaidia sisi kuitoa klabu yetu hapa ilipofikia na kwenda mbele kwa kushirikiana pamoja,” amesema Popat.
Kwa upande wake, Dk. Tiboroha, amesema katika muundo wa klabu ya Azam, kuna timu zote, kubwa, vijana kwa maana academy, hivyo makujumu yake yatakuwa ni kusimamia vitu mambo yote.

Kwa upande wake, Dk. Tiboroha, amesema katika muundo wa klabu ya Azam, kuna timu zote, kubwa, vijana kwa maana academy, hivyo makujumu yake yatakuwa ni kusimamia vitu mambo yote.

“Majukumu yangu ni kuangalia na kusimamia nini kinachoendelea na kuhakikisha yale malengo ya Azam FC ambayo ni ushindani na kuendeleza vijana yanafanikiwa,” amesema Dk. Tiboroha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles