28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Slaa: Mkataba wa Bandari siyo jambo geni Tanzania

Balozi Mstaafu Dk. Wilbrod Slaa amesema kuwa mkataba wa bandari siyo jambo geni kwa Tanzania na kwamba imesaini mingi.

Dk. Slaa ameyasema hayo leo Jumanne Juni 13, 2023 jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

“Nikirejea kwenye suala la MOU na “ Intergovernmental Agreement” hili si jambo geni nchini Tanzania. Memorandum of Understanding” ni “makubaliano ya awali” ambayo pande mbili zinazotaka kuingia kwenye mkataba na kwa kawaida Serikali moja na nyingine zinatia saini.

“”MOU hufuatiwa na mkataba unaoitwa Intergovernmental Agreement au kwa kifupi IGA. Hivyo mkataba huu si wa kwanza kwa Serikali ya Tanzania,” amesema Dk. Slaa.

Dk. Slaa, ambaye aliwahi kuteuliwa na Hayati Dk. John Magufuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden, amefafanua Tanzania imesaini maelfu ya mikataba ya uwekezaji kati yake na mataifa mengine.

Akitolea mfano, amesema kuwa Tanzania imesaini jumla ya mikataba 2,829 ya uwekezaji, yaani “Bilateral Investment Treaties (BITS)”, na nchi za kigeni mbalimbali.

Kati ya mikataba hiyo ya BITS, jumla ya mikataba 2,219 inaendelea kutumika hadi sasa na mikataba yenye maslahi ya kibiashara ni 435 na ambayo inatumika ni 264,” amesema Balozi Dk. Slaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles