28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

BASATA kuja na muongozo wa maadili katika kazi za sanaa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) linatarajia kuja na muongozo wa maadili katika kazi za sanaa unaolenga msanii, mtunzi, mameneja na wengine na kutoa elimu kwa wasanii kuhusu muongozo huo.

Hayo yameelezwa leo Juni 13, 2023 jijini Dar es Salaam, na Katibu Mtendaji wa BASATA, Dk. Kedmon Mapana wakati akibanisha vipaombele vya Baraza hilo kulekea mwaka wa fedha 2023/2024.

Ametaja vipaombele hivyo kuwa ni kukuza, kufufua na kuendeleza sanaa nchini ikiwemo mazingaombwe na sanaa za majukwaani nakwamba wanahitaji kufanya kazi ya ziada ili hayo yatimie ikiwamo kudhibiti maadili.

“Suala la maadili katika kazi ya sanaa tunalipa kipaumbele kuhakikisha kazi zenu haivunji heshima ya mtu, hazina upotoshaji, hazichochei, hazishawishi uhalifu na mambo mengine,”amesema Dk. Mapana.

Amesema kwa sasa wapo katika kupitia upya kanuni za Baraza hilo na kufanya marekebisho ili ziwe wezeshi na siyo dhibiti.

Aidha, Dk. Mapana amebaini kuwa wana mipango mbalimbali ikiwemo kuanzisha mdundo wa Taifa, kivunge cha mtozi ili watozi wao waweze kuzalisha midundo mbalimbali na kubuni amapiano za Kitanzania kama nchi zingine.

Amesema wasanii wakienda kufanya maonyesho nje ya nchi watakuwa wanalipia kibali ambacho ni Sh 50,000 na Baraza hilo litaendelea kuwatafutia masoko.

Dk. Mapana amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha wanatarajia kuanzisha ‘BASATA Vibe na jukwaa la Serengeti ili wasanii wapate uwanja wa kupeleka nje ya nchi kuuza kazi zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles