29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Shein: Serikali zetu zitaendelea kudumisha usalama, upendo na amani

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amewahakikishia wananchi wote kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na ya rais John Magufuli kulinda usalama wa nchi na kudumisha upendo na amani.

Ametoa kauli hiyo leo Januari 12, 2019 katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Gombani Chakechake huko Pemba ikiwa na kauli mbiu ya “Mapinduzi yetu ndio umoja wetu tuyalinde kwa maendeleo yetu”.

“Ninawahakikishia kuwa nchi yetu iko salama na itaendelea kubaki salama na serikali zetu mbili zitaendelea kutimiza majuku yake ipasavyo na tutahakikisha amani na utulivu vinadumishwa na sheria zote zinafuatwa.

“Mimi na rais Magufuli tutahakikisha Muungano wetu unadumu kwa dhamira ile ile ya viongozi wetu waliopita ili nchi yetu izidi kubaki na amani,” amesema.

Naye Makamu wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amempongeza rais Magufuli kwa juhudi na mwenendo wake wa utunzaji wa amani na kuboresha uchumi.

“Lengo kuu la Mapinduzi ya Zanzibar lilikuwa ni kumkomboa Mzanzibar na sisi tunaendelea kuyathamini mapinduzi haya kwani ndiyo chanzo cha maendeleo tuliyonayo sasa,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles