25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwanjelwa awafunda watumishi wa umma

Mwandishi Wetu -Singida

WATUMISHI wa umma nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufanikisha juhudi za Rais Dk. John Magufuli za kukuza uchumi.

Hayo yalisemwa jana mjini Singida na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, alipokuwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida katika ziara ya kikazi mkoani hapa.

Dk. Mwanjelwa alisema kuwa ni lazima watumishi wa umma waheshimu kazi na wahakikishe wanatimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano haitovumilia watumishi wazembe.

“Mtumishi wa umma ni tunu, kwa hiyo ni bora ukachezea mshahara kuliko kuchezea kazi kwa sababu wapo wanaotamani kuingia serikalini, lakini hawana fursa hiyo,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Alitoa wito kwa watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya Rais Magufuli na si kwa kulegalega.

Alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano ni ya uadilifu, utendaji kazi uliotukuka na haiko tayari kumwonea mtumishi yeyote.

Pia aliwataka watumishi kuwa na subira katika kipindi ambacho Serikali inafanyia kazi changamoto zao za malimbikizo ya mishahara, kupandishwa madaraja na nyinginezo.

Dk. Mwanjelwa yupo katika ziara ya kikazi mkoani Singida kwa lengo la kukagua utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na kukutana na watumishi kwa lengo la kusikiliza maoni na kutatua kero zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles