24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Gwajima azindua Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO)

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima amezindua Baraza jipya la Mashirika Yasiyo ya kiserikali linalojumisha wajumbe kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wapya wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma

Dk. Gwajima amezindua Baraza hilo leo Juni 10, 2021 jijini Dodoma mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi wa Baraza uliosimamiwa na Kamati ya mpito iliyoteuliwa na Waziri huyo Juni 7, 2021.

Waziri Dk. Gwajima amesema kuwa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni chombo cha uwakilishi na kiungo muhimu kati ya Mashirika na Serikali, hivyo uwepo wa Baraza hili utasaidia utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa Sheria.

“Niliamua kutekeleza Sheria kwa kuteua Kamati ya Mpito ya uchaguzi wa Baraza hili kwa sababu mimi kama msimamizi wa Sheria na Kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nisingeweza kuvumilia vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na Kanuni hizo” alisema Waziri Dkt. Gwajima.

Pia Waziri Dk. Gwajima ametoa wito kwa viongozi wa wajumbe wote wa Baraza kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na uzalendo wa hali ya juu kwa sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Taifa kwa ujumla ili kuhakikisha Sekta hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.

“Uchaguzi umeshaisha sasa nendeni mkafanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ilioyopo ili kukidhi matarajio ya waliochagua na jamii ya Watanzania kwa ujumla” alisema Waziri Dk. Gwajima

Aidha, Dk .Gwajima ameliahidi Baraza hilo kutekeleza mapendekezo yao na kuwataka wajitoe kwa hali na mali kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha yale yaliyopendekezwa yanafanyiwa kazi kwa kasi na weledi.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Idara kuu ya Maendeleo ya jamii, Dk.John Jingu amesema matarajio ya Wizara ni kuhakikisha NaCoNGO inafanya kazi kwa waledi na kusaidiana na Serikali katika kutatua changamoto za watanzania katika maendeleo .

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali, Dk. Lilian Badi amesema uongozi mpya utahakikisha panakuwa na uwajibikaji, na kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu wa Baraza hilo na kujenga mahusiano na taasisi zingine pamoja na kuzingatia Sheria zilizowekwa.

Akitoa maelezo ya uchaguzi Mwenyekiti wa Kamati ya mpito ya uchaguzi wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Wakili Flaviana Charles amesema mchakato wa uchaguzi ulifanywa kwa kuzingatia kanuni na demokrasia na imewezesha kupata viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi taifa.

Aidha ameainisha mapendekezo kwa Baraza jipya kuwa ni pamoja na kuweka ratiba mapema ya chaguzi zijazo, uwiano wa uwakilishi, kuwa na data base, kuwajengea uwezo zaidi watumishi wa NaCoNGO na kupitia kanuni zilizopitwa na wakati pamoja na kuwepo bajeti toshelezi ili kuweza kuendesha Baraza hilo kwa ufanisi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles