22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto watuhumiwa kumkata viungo mama yao na kumzika

Na Nyemo Malecela – Kagera

BIBI Frazia Rukera (99) mkazi wa kijiji cha Mkombozi, Nkwenda wilayani Kyerwa mkoani Kagera ameuawa na kuzikwa bila kichwa, mguu mmoja na mkono mmoja baada ya wauaji kutokomea na viungo hivyo.

Kufuatia tukio hilo lililotokea Julai 7, mwaka huu saa 10 alfajiri nyumbani kwa marehemu, Jeshi la Polisi linaendelea kuvisaka viungo vya marehemu ambaye tayari ameshazikwa.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Tuntufye Mwakagamba amesema hadi sasa wanawashikiria watuhumiwa watatu wa tukio hilo ambao ni watoto wake wa kuzaa, Laurent Francis (60) mkulima, Alexanderea Francis (55) mkulima na mkwe wake Agnes Gidion (70).

“Tunawashikiria watuhumiwa hao kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mama yao mzazi kutokana na kumtuhumu kwa muda mrefu kuwa bibi huyo alikuwa mchawi/mshirikina na kuwa amekuwa akiwaloga wao na familia zao ugomvi uliowafanya watoto hao kumtenga mama yao bila kumpa msaada wowote.

Siku ya tukio, bibi huyo alikuwa amelala peke yake alivamiwa na watu ambao bado hawajafahamika hadi sasa na kumuua kwa kumkatakata na kitu chenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake hadi kifo chake na kutenganisha baadhi ya viungo vya mwili na kuvitoa nje na kuvitelekeza.”

Tuntufye alisema baada ya bibi huyo kutengwa na watoto hao alibaki akitegemea msaada wa mtoto mmoja, Thomas Francis ambaye alitengana na mke wake Agnes Gidion (mtuhumiwa namba tatu) na baada ya ndoa yao kuvunjika mke huyo alimtamukia mumewe kuwa “umeniacha lakini nitakuja kufanya jambo kwenye familia yenu lisilo sahulika”.

“Kufuatia kauli hiyo, jeshi la polisi linamshikiria mwanamke huyo kwa ajili ya kujua undani wa kauli yake aliyoitoa kwa mume wake,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles