24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

DIT, BORA kuanza kushirikiana

Mwandishi Wetu

Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Profesa Preksedis Ndomba ametembelea Kampuni ya kutengeneza viatu ya BORA ikiwa ni hatua za awali katika kuingia ushirikiano.

Katika ziara hiyo, Profesa Ndimba ameambatana na Mkurugenzi wa Kampasi ya DIT Mwanza, Dk Albert Mmari, na Mkuu wa Idara ya Mafunzo Viwandani Dk John Msumba.

Timu hiyo kutoka DIT imepata nafasi ya kutembelea kiwanda hicho cha BORA kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho ambapo DIT Kampasi ya Mwanza inatoa mafunzo ya uchakataji ngozi ikiwa ni pamoja na utengenezaji viatu, itanufaika kwa wakufunzi wake kuongeza ujuzi na utaalamu kiwandani hapo na pia wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza kwa vitendo katika kiwanda hicho na kwa upande wa kiwanda watanufaika kwa kupata wataalamu kutoka DIT.

Kwa mujibu wa Profesa Ndomba, DIT kupitia kampasi ya Mwanza inalenga kuwa kituo cha umahiri katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi na teknolojia zake ambapo Mkurugenzi Mkuu wa BORA, Rajesh Sajinan aliahidi kushirikiana na DIT ili kupata wataalamu.

 Makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo yatatiwa saini hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu muhimu za kiutendaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles