27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Diamond, Zari kimeeleweka

NA CHRISTOPHER MSEKENA

HATIMAYE staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake, Zarina Hassan a.k.a  Zari The Boss Lady, wamemaliza tofauti zao huku wakitarajia kuboresha njia za kuwatunza pamoja watoto wao, Tiffah na Nillan.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Zari kumshambulia Diamond Platnumz kwa kutangaza kuzilipia kodi ya miezi mitatu familia 500 ilhali hatoi matunzo kwa wanawe hao wanaoishi na mama yao Afrika Kusini.

Akizungumza mapema jana, jijini Dar es Salaam, Diamond Platnumz alisema yeye na Zari wamekuwa hawana uhusiano mzuri kwa muda mrefu ila juzi alimtumia meseji na wakamaliza tofauti zao.

“Mnapokuwa kwenye mahusiano halafu mkatengana kidogo na mkawa na watoto, kunakuwa na mikwaruzano na kila mtu anakuwa na hasira na jinsia za wenzetu ndio wanakuwa na hasira zaidi kwa sababu wanabaki na watoto.

“Mimi na yeye tumekuwa hatuzungumzi, tulikuwa tunazungumza kupitia mwanasheria, nilivyoona vile jana, nikamtumia meseji kistaarabu, nikamwambia wewe ni mzazi mwenzangu, tena wa kipekee sababu umenizalia mtoto wangu wa kwanza, kwahiyo heshima yangu kwako ni kubwa sana, hivyo jitahidi kuepuka migogoro ambayo haina sababu kwenye mitandao, haileti picha nzuri, baada ya hapo, tukaanza kuongea na kila mmoja akatoa duku duku lake,” alisema Diamond.

Aliongeza kuwa kabla ya kuamua kuwasiliana na Zari kwa mara ya kwanza tangu waachane, alipanga kumjibu kupitia mtandao, ila uongozi wake ukamkataza.

“Nilipaniki nikaandika bonge la meseji, nikataka nipeleke mjini (niposti mtandaoni), viongozi wakasema haileti maana nikae tu kimya, nikaona nizungumze naye, yeye akatoa yake ya moyoni, akasema labda hakukuwa na mazungumzo mazuri baina ya wanasheria wetu, tukazungumza vizuri na mambo ya corona yakipita, suala letu la uleaji wa watoto litakuwa limeboreshwa,” alisema Diamond.

Hali kadharika, Diamond aliongeza kuwa baada ya zoezi la kuzilipia kodi familia 500, atakuja na mpango wa kuwapa chochote kitu madj wote ambao kipindi hiki cha janga la corona kazi zao zimesimama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles