22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

DHAHABU, MAGARI YA BILIONI TANO YATAIFISHWA

Fredy Azzah, Dodoma    |  


Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kwa mwaka wa fedha 2017/18, mali yakiwamo magari na dhahabu zenye thamani ya Sh bilioni 5.68 kutoka kwa washtakiwa waliotiwa hatiani zilitaifishwa.

Kati ya mali hizo, amesema dhahabu ilikuwa kilogramu 24.5 zenye thamani ya Sh bilioni mbili na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na Audi yaliyokamatwa katika Bandari ya Dar es Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba.

“Aidha, tumetaifisha fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya Sh milioni 908 na fedha zilizotozwa kwa washtakiwa hao kama faini kiasi cha Sh bilioni 2.4, pikipiki 34, mafuta, mashine za kuhesabia fedha na basi la abiria lililokuwa likitumika kusafirishia meno ya tembo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Profesa Kabudi amesema wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2017/18 ilipokea maombi 14 ya kurejesha watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai waliopo katika nchi za Rwanda, Zambia, Kenya, Malawi, Marekani na Uingereza.

“Wizara pia katika kipindi hicho iliwasilisha maombi manne ya kurejeshwa nchini kwa watuhumiwa wanaokabiliwa na makosa mbalimbali waliopo katika nchi za Rwanda, Uganda, Zambia na Afrika Kusini,” amesema.

Prifesa Kabudi amesema makosa hayo yalihusisha makosa ya usafirishaji wa dawa za kulevya, mauaji ya kimbari, wizi, mauaji, makosa ya kimtandao na ubakaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles