NA CHRISTOPHER MSEKENA
KUTOKA nchini Ufaransa mwanamuziki, Desclo James W a.k.a Desclo J, amerudi kivingine na wimbo, Sape Comme Un Z aliomshirikisha rapa nyota kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Gaz Fabilouss.
Desclo J, ameliambia MTANZANIA kuwa lengo la kufanya ngoma na Gaz Fabilouss ni ukubwa wa msanii huyo nchini Kongo hivyo anaamini atapata mashabiki wapya katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati.
“Muda wowote kutoka sasa video ya Sape Comme Un Z itakuwa kwenye chaneli yangu ya YouTube na mitandao mingine ya kuuza na kununua muziki kama vile Spotify, iTunes, Apple Music, Deezer na mingine yote, huu ni mzuri wa kitofauti kabisa,” alisema Desclo J.