23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yapongezwa mapambano ya Ukimwi, juhudi zaidi zahitajika

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Tanzania imepongezwa kwa hatua ambazo zimefikiwa katika kukabiliana na janga la virusi vya ukimwi.

Hayo yalisemwa juzi na Balozi wa Marekani nchini, Dk. Donald Wright katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duninia yalitofanyika Desemba mosi, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Alisema kumekuwa na mafanikio makubwa nchini katika kukabiliana na virusi vya ukimwi ikilinganishwa na miaka ya nyuma jambo ambalo linatokana na mkazo mkubwa uliowekwa na serikali.

“Nina bahati ya kuwa hapa leo nikiwakilisha sio tu serikali ya Merekani, lakini pia Kundi pana la Washirika wa Maendeleo juu ya VVU na UKIMWI.

“Kundi hili linajumuisha washirika na wafadhili wote wa nchi mbili, pamoja na Mpango wa dharura wa Rais wa Merekani wa Usaidizi wa UKIMWI (PEPFAR), Mfuko wa Ulimwenguni na Sekretarieti ya UNAIDS na Cosponsors.

“Mkutano huu unaingiliana na serikali ya Tanzania – kupitia TACAIDS na NACP – kuhakikisha msaada wa kiufundi na ufadhili wa majibu kamili ya VVU hapa Tanzania.

“Ni wazi kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kufikia udhibiti wa janga hili na kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi, pamoja na mafanikio hayo ninahimiza Tanzania ifanye upya mtazamo wake juu ya kinga ya msingi haswa kwa wasichana na wanawake,” alisema Balozi Wright.

Balozi Wright  alisema Wanawake na wasichana bado wana mzigo mkubwa wa janga la VVU nchini ambapo alisema kwa mujibu wa ripoti ya UNAIDS, ya mwaka  2019, kati ya maambukizi mapya ya VVU 77,000 nchini Tanzania, asilimia 60 walikuwa ni  wasichana na wanawake,lakini pia kukabiliana na maambukizi ya kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto jukumu ambalo alisema jitihada za kila mmoja zinahitajika.

“Lazima tuongeze juhudi zetu za kufikia wanawake wakati wa utunzaji wa ujauzito na kuhakikisha kuwa mama na mtoto wanafuatiliwa kila wakati ili kuhakikisha watoto wanazaliwa bila VVU,” alisema Balozi Wright.

Akizungumzia matumizi ya kondomu, Balozi Wright alisema kuwa njia ya kuzuia maambukizi ya ukimwi zinatakiwa kupatikana kwa urahisi kwa watanzania wote.

Aidha, aligusia kukosekana kwa usawa wa kijinsia ambapo alisema kuwa jambo hilo linapaswa kushughulikiwa.

“Kukosekana kwa usawa wa kijinsia na unyanyasaji wa kijinsia unapaswa kushughulikiwa kupitia njia ya kitamaduni na pana, kufikia kudhibiti janga itakuwa mafanikio mazuri kwani tungeokoa maisha ya watu wengi.

“Lakini,bado kuna kazi ya ziada inatakiw akufanyika katika kuhakikisha kuwa tunafikia malengo ya 95-95-95. Tena, tunazo zana za kufanya hili liwe kweli,” alisema balozi huyo.

Aidha, alisema kuwa lazima Tanzania iendelee kutoa tiba ya kuzuia TB ili kupunguza vifo kati ya watu wanaoishi na VVU.

“Ninataka pia kuwakumbusha ukweli mbaya kwamba kwamba watu wanaoishi na VVU bado wanapata unyanyapaa na ubaguzi.

“Kwani kupata ukwimwi siyo mwisho wa maisha siku hizi hata ukiwa na ukwimwi na ukazingatia masharti ya dawa bado utaishi muda mrefu tena maisha yako yatakuwa na afya na amani tofauti na mitazamo hasi ya watu,” alisema Balozi Wright.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles