24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mtanzania, Rai, Bingwa, Dimba kusitisha uzalishaji kwa muda

Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya New Habari2006 LTD inayozalisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Bingwana Dimba imetangaza kusitishauzalishaji wa magazeti yote kwa
muda kutokana na mwenendo mbaya wa biashara hivyokushindwa kujiendesha.


Kutokana na hali hiyo uongozi umesema kuwa watatumia
muda huo kujipanga na kuimarisha maudhui ya habari huku
mitandao ya kijamii ya Mtanzania Digital ikiendelea kufanyakazi kama kawaida.


Akizungumza jana na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mhariri Mtendaji, Dennis Msacky leo Ijumaa Desemba 4, amesema uzalishaji wa
magazeti hayo utakoma kuanzia
Jumatatu.


“Usitishaji wa magazeti ni wamuda, lakini pia katikan muda ambao magazeti yatakuwa hayachapishwi, Mtanzania Digitalna mitandao yake yote ya kijamiiitaendelea kuwa hewani.


“Mwaka mmoja na nusu uliopita kampuni ilipunguza wafanyakazi lakini tangu kipindi hichohali haijakaa sawa, uzalishaji unaendelea kushuka.
“Uamuzi wa wenye kampunini kwamba kuanzia Jumatatu hakutakuwa na uzalishaji wa gazeti lolote kwa maana hiyo uzalishaji unasitishwa kwa muda hadi hapo baadaye.

“Kuanzia kesho kila mfanyakazi atahakiki stahiki zake
zote, sambamba na hilo pia tutapunguza wafanyakazi ambao kila
mmoja atalipwa stahiki zake kwa mujibu wa sheria, mchakato wa
malipo utafanyika mara moja kuanzia kesho,” amesema Msacky.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles