Jack Manasi aimwagia sifa ‘Zungusha’

0
504

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MWANAMUZIKI anayefanya vizuri kwenye muziki wa Injili nchini Australia, Jack Manasi, amesema sababu za wimbo wake mpya, Zungusha kufanya vizuri ni ladha mpya aliyoiimba.

Akizungumza na MTANZANIA, Manasi alisema katika wimbo huo amechanganya ladha ya muziki wa rhumba na singeli hivyo umekuwa na ladha tamu kwenye masikio ya wapenzi wa muziki wa gospo.

“Mungu amenipa uwezo wa kuimba muziki wa aina yoyote ili ujumbe wake uwezo kuwafikia watu, ndio maana kwenye Zungusha nimeimba tofauti na vile wengi walivyodhani ila nashukuru watu wanabarikiwa, tayari wimbo unapatikana kwenye chaneli yangu ya YouTube, Deezer, Audiomack, Boomplay, iTunes, Spotify na Amazon Music,” alisema Manasi maarufu kama Australian Boy.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here