24 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

De Gea amuomba radhi Schmeichel

 MANCHESTER, ENGLAND 

MLINDA mlango wa timu ya Manchester United, David de Gea, amemuomba radhi mlinda mlango wa zamani wa timu hiyo Peter Schmeichel baada ya kuvunja rekodi yake. 

Juzi Manchester United ilishuka dimbani kwenye Uwanja wa Villa Park dhidi ya wapinzani wao Aston Villa na kuwachapa mabaoa 3-0. 

De Gea alikuwa langoni na kupambana kuzuia mipira ya hatari, hivyo mchezo huo ulikuwa wa 399 kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29 akiitumikia timu hiyo. 

De Gea alijiunga na klabu hiyo ya Manchester United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid. Tangu hapo kipa huyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho na mchezo wa juzi umevuka michezo iliyochezwa na Schmeichel ambaye alikuwa hapo tangu mwaka 1991 hadi 1999. 

Hata hivyo, bado De Gea ana safari ndefu kuweza kuifikia rekodi ambayo imewekwa na nyota wa zamani wa timu hiyo Ryan Giggs, ambaye anatajwa kuwa mchezaji ambaye amecheza michezo mingi ndani ya Old Trafford akicheza jumla ya michezo 963, tangu mwaka 1990 hadi 2014 alipostaafu soka. 

Kutokana na hali hiyo De Gea amemuomba radhi Schmeichel kwa kuvunja rekodi yake ambayo aliiweka kipindi hicho. 

 “Samahani kwa Schmeichel, lakini kwangu hili ni jambo kubwa na lenye furaha, ukweli ni kwamba nipo hapa kwa muda mrefu na nimekuwa nimepata nafasi kubwa ya kucheza, hivyo najivunia na hatua hiyo na nina furaha kuwa kwenye klabu kubwa kama hii na kucheza michezo mingi, ninaamini nina michezo mingine 400 inakuja,” alisema mlinda mlango huyo. 

Manchester United wanapambana kuhakikisha wanaingia kwenye nafasi nne za juu ili kuweza kufuzu kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na sasa wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 34 baada ya mchezo wa juzi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles