26.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

De Bruyne aipa ubingwa Liverpool

LONDON, ENGLAND

KIUNGO wa Manchester City, Kevin De Bruyne, anaamini timu ya Liverpool  inaweza kutwaa ubingwawa Ligi Kuu England msimu huu iwapo itaendelea kuonyesha kiwango bora wanachokionyesha hadi mwisho wa msimu.

De Bruyne, ambaye kwa sasa amerejea uwanjani baada ya wiki sita za majeraha ya kifundo cha mguu, hana hofu na kiwango cha Liverpool kama itatwaa ubingwa msimu huu.

Manchester City ilimaliza msimu uliopita na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 19 dhidi ya Liverpool lakini De Bruyne anaamini  kitendo hicho hakitatokeamsimu huu.

“Sijui kwanini wanakua hawana mwendelezo wa kiwango chao, lakini safari hii wanaweza kumaliza msimu wakiwa katika ubora wao.

“Sina wasiwasi juu yao, watafanya kwa kiwango chao na sisi tutajaribu kushinda michezo yetu na kusonga mbele. Wao watajaribu kutukimbiza na hiyo itakuwa kinyume chake kwetu.
“Lakini bado mapema. Hatuna haja ya kuwa na presha, tunatakiwa kufanya kile tunachotakiwa kukifanya.”

Liverpool na Manchester City zilitoka suluhu zilipokutana Oktoba mwaka huu katika Uwanja wa Etihad, lakini zinatarajia kuvaana tena Januari mwakani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,340FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles