Wasafi Festival yapigwa ‘stop’ Diamond, Rayvan wafungiwa kwa muda usiojulikana

0
2141


Bethisheba Wambura, Dar es Salaam

Baraza la Sanaa ta Taifa (BASATA) limewafungia wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasib Abdul (Diamond Platinum) na Raymond Shaban (Rayvan) kutokufanya onyesho lolote ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana kuanzia leo Decemba18, 2018 kwa kukaidi agizo la kutoendelea kuutumia wimbo wao unaojulikana kwa jina la ‘Mwanza’

Wimbo huo ulifungiwa na Baraza hilo Novemba 11, 2018 baada ya kuonekana kuwa na maneno yanayokiuka maadili ya Mtanzania.

Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa na
Onesmo Kayandakwa kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mungereza ni kwamba, Baraza hilo pia limesitisha kibali cha Tamasha la Wasafi Festival2018 kutokana na ukiukwaji wa Sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa tamashahilo nchini.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo umetokana na wasanii hao kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018 chini ya uongozi wa NasibAbdul (Diamond Platinumz).

“Baraza limefikia uamuzi wa kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hao kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia masuala ya sanaa nchini na uvunjifu wa maadili uliokithiri unaofanywa na waandaaji wa Tamasha la Wasafi 2018 chini ya uongozi wa Nasib Abdul (Diamond Platinumz),” imeeleza taarifa hiyo .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here