DC WA CHEMBA ANUSURIKA KIPIGO

 

Na Mwandishi wetu,

Mkuu wa Wilaya ya Chemba-Dodoma, Simon Odunga anusurika kipigo kwa madai ya kuwakataza wananchi wa kijiji cha Mlongia kulima eneo ambalo linadaiwa ni la mwekezaji. 

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Baraza la Kijiji, Salum Ikanda, sakata hilo ni baada ya DC huyo kuwataka wananchi waondoke eneo hilo la ekari 500 mara moja ili kumpisha mwekezaji.

Tukio hilo liliambatana na mkuu huyo kuamuru Mwenyekiti wa Kijiji akamatwe jambo ambalo liliwafanya  wananchi kujawa hasira na kuanza kuushambulia msafara wake.

DC Odunga alilazimika kukimbia baada ya gari lake kupigwa mawe pia baadhi ya viongozi wa wilaya akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri walilazimika  kukimbia pia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here