25.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

DC: Viongozi wa mitaa uendeshaji miradi si kazi yenu

Tunu Nassor -Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori, amewataka viongozi wa mitaa kutokuingilia uendeshaji wa miradi ya maji ya jamii kwa kuwa si kazi yao.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa maji safi wa Saranga Ijumaa Machi 22 amesema viongozi wa mitaa wao ni walezi wa miradi uendeshaji si kazi yao.

“Kuna baadhi ya maeneo tumezindua miradi kama hii lakini baadhi ya viongozi wa mitaa wanataka kuendesha, hii ni kazi ya kamati za maji,” amesema.

Aidha amewapongeza Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasa ) kwa kukamilisha mradi huo ndani ya miezi  mitatu.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha udhibiti Ubora wa Dawasa mhandisi Christian  Christopher amesema mradi huo umesanifiwa vyema kuhakikisha kuwa unadumu na huduma inayotoleta kwa wananchi inakuwa ni bora.

“Mabomba tumelaza kwa utaratibu unaotakiwa na kuhakikisha yanaishi muda mrefu ili serikali isiingie gharama nyingine kuwekeza upya katika huduma hii,” amesema Christopher. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,784FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles