23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Rais Bongo kurejea Gabon leo

LIBREVILLE, GABON

IKIWA imepita miezi mitano tangu aondoke nchini mwake Gabon, Rais Ali Bongo, anatarajiwa kurejea nchini humo mwishoni mwa wiki hii kutoka Morocco ambako alikuwa amelazwa kutokana na kuugua maradhi ya kiharusi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Ofisi ya Rais, Ike Ngouoni, kiongozi huyo anatarajia kuondoka Morocco leo.

“Tunapenda kuwataarifu kuwa mwananchi mwenzetu, Rais Ali Bongo, anatarajia kurejea nyumbani leo, wananchi wote wanaalikwa kumpokea na kumshukuru Mfalme wa Morocco Mohammed wa sita kwa uungwana na sapoti yake aliyoitoa kwa kiongozi wetu kipindi chote alichokuwa anaugua,” ilisema taarifa hiyo na kukaririwa na Shirika la Habari la Al Jazeera.

Bongo mwenye umri wa miaka 60, aliondoka Gabon mnamo Oktoba 24, mwaka jana kuelekea nchini Saudi Arabia kwa ziara ya kikazi, lakini aliugua ghafla hivyo kupelekwa kwenye matibabu nchini Morocco.

Tangu wakati huo alirejea nchini mwake Gabon mara mbili, lakini hakukaa kwa zaidi ya muda wa saa 48 katika safari zote, ingawaje Serikali imesisitiza kuwa hali yake kiafya ni njema.

Mapema Februari mwaka huu, rais Bongo aliongoza kikao cha baraza la mawaziri wakati ambao alitangaza uteuzi na kuwaondoa baadhi ya wasaidizi wake wa karibu, huku vyombo vya habari vikinyimwa mwaliko wa kuhudhuria tukio hilo.

Mapema Januari 7, mwaka huu Gabon imeshuhudia jaribio la mapinduzi dhidi ya utawala wa rais Bongo, hali ambayo imetafsiriwa kutokana na ombwe la uongozi linaloikabili nchi hiyo.

Bongo aliingia madarakani mwaka 2009 kufuatia kifo cha baba yake, Omar Bongo, ambaye alichukua madaraka ya urais mwaka 1967.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles