22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

DC Mufindi aagiza kulindwa kwa vyanzo vya maji

Na Raymond Minja

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mkoni Iringa, Jamhuri William amewataka viongozi wa Kata, tarafa na vijiji kuhakikisha wanasimamia vyema na kulinda vyanzo vya maji ili kupunguza uharibu wa vyanzo hivyo.

Wiliam ametoa agizo hilo wakati wa kutembelea chanzo cha maji katika kijiji Ludilo kata ya Mdabulo na kukuta kuwepo kwa uharibifu mkubwa kwenye chanzo cha maji.

Alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakiwaona wananchi wanalima hadi kwenye vyanzo vya maji bila kuchukua hatua zozote hali ambayo imepelekea kuwepo kwa uharibifu huyo.

“Ili kurekebisha hali hii ya uharibifu wa vyanzo vya maji iliyojitokeza naagiza katika vyanzo vyote ambavyo vimevamiwa kuanza mara kupanda miti ya mivengi ili kulinda vyanzo hivi.”Alisema Wiliam.

Aidha, William amelishukuru shirika la maendeleo vijiji(RDO) kwa hatua ambazo wamekuwa wakizichukua kulinda vyanzo hivyo ambapo hadi sasa wamepandikiza miche 5000 ya mti ya mivengi kwa lengo la kupanda.

Wiliam amewataka wananchi ambao wameshiri uharibifu huo wa vyanzo hivyo vya maji kushirikia katika zoezi la upandaji miti katika vyanzo hivyo vya maji.

“Nataka kuwaambia wananchi wangu wale wote walioshiriki kuharibu vyanzo hivi nao washiriki kupanda miti hii pamoja na kuitunza hadi pale watakapovuna mazao yao na kisha kuondoka katika vyanzo hivi na kuviacha vikiwa salama,” alisema.

Kwa upande wake Mratibu Mradi wa shirika la maendeleo vijijini, Fidelis Filipatali alisema kuwa jumla ya wakazi elfu kumi na moja watanufaika na mradi huo.

Mratibu huyo alisema kuwa changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo ni pamoja na michango hafifu kwa wanufaika wa maji kutokana na mitazamo hasi na Elimu potofu kwa jamii

“Kumekuwepo na mitazamo hasi na Elimu potofu inayotolewa kwa wananchi juu ya suala la uchangiaji wa huduma za miradi ya maji kwa sababu jukumu la uendelezwaji wa miradi hii ya maji ni wanufaika wenyewe.” Alisema Filipatali

Hata hivyo, Filipatali alisema kuwa miradi hiyo ya maji itagharimu kiasi cha Sh milioni 9 hadi kukamilika

“Fedha hizi fedha ni ufadhiri kutoka kwa watu wa Australia ambao wametusaidia fedha hizi kwa sababu hata wao ni wakulima kama sisi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles