30.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

DC agomea misaada ya wadau Rorya

*Ni madawati, vitanda vya hospitali toka kwa wadau, mwenyewe avunja ukimya

Na Mwandishi Wetu, Rorya

KATIKA hali ya kushangaza Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Juma Chikoka anadaiwa kukataa kupokea misaada ya maendeleo wilayani kwake kwa kile kinachoelezwa kuwa mtifuano wa kisiasa huku mwenyewe akikanusha madai hayo.

Hatua hiyo inatokana kukataliwa misaada hiyo inatokana na hofu ya hali ya kisiasa huku ikidaiwa kuwa wadau hao wa maendeleo huenda wana nia ya kuwania jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo kwa sasa Jimbo la Rorya linaongozwa na Mbunge Jaffari Chege.

Wadau hao wa maendeleo jana walianza kazi ya kukabdhi misaada hiyo katika maeneo mbalimbali wilayani Rorya ambapo misaada imepatikana kwa kushirikiana na marafiki zao wamekuwa na zoezi ya kugawa madawati 20 kwa kila shule kwenye shule zote za msingi 132 zilizopo wilayani Roya kama hatua kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan.

Katika kile kinachoelezwa hofu ya kisiasa DC Chikoka, anadaiwa kugoma kutokabidhiwa kwa madawati hayo zaidi ya 800 kwenye shule zote hizo jambo ambalo limezua sintofahamu wilayani hapa.

Wadau hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa zamani ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Rorya, Sango Kasera, ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, waliendesha harambee kwa kushirikiana na wadau wengine waliopo maeneo mbalimbali nchini ambapo wamefanikiwa kupata madawati pamoja na vitanda 60 kwa ajili ya kusaidia zahanati na vituo vya afya hapa wilayani Rorya.

Akizungumzia hali hiyo Diwani wa Kata ya Komuge, William Nestory Marwa alisema kuwa katika hali ya kushangaza jana alipewa taarifa na mtendaji wake wa kata ambaye aliitisha kikao na viongozi wote wa ngazi ya kata na kutoa maagizo ya kutopokelewa kwa misaada hiyo.

“Wajumbe wa kamati ya siasa pia amewaambia kuwa amepewa onyo na DC kutopokea misaada hii, lakini naye nikamwambia basi mwambie Malengu (Katibu kata wa CCM) aje kupokea naye akaniambiaamepewa onyo hakuna viongozi wa CCM kuingia.

“Hivi mimi nimebaki hoi ninauliza shida ni nini malengo amesema ameambiwa amepewa hela na wewe (Sango) ya kufanya sherehe yake ya kubariki ndoa, nikaema mimi siwezi kuacha kuja naye mtendaji wangu wa kata ananiamba hawezi kukanyaga (kuja) sasa nauliza kuna shida gani, ameniambia DC amesema yeye amepokea madawati na amezindua na hakuna mtu mwingine wa kuja kufanya hivyo.

“Hata mratibu wa elimu nimemwambia nenda pale kwa kuwa hao wadau wamefika naye ananiambia nimetoka kidogo, nikabaki namuuliza sasa tunafanyaje. Kwani wanawaza nini kwani unagombea ubunge kwa kupiga kampeni?,” amesema na kuhoji Diwani huyo.

Amesema kuwa anashangazwa kuwa onyo hilo la kutopokea madawati hayo linatokana na nini.

“Mimi ninawashukuru nyinyi kama wadau wa maendeleo katika Wilaya yetu ya Rorya na kwa hakika madawati yamefika na mmeniokoa na adha waliyokuwa wanaipata wanafunzi katika shule za kata yanu,” amesema.

Pamoja na hali hiyo Wilaya ya Rorya pia imebainika kuwa na uhaba wa matundu vya vyoo katika shule zake huku baadhi ya majengo hayo ya vyoo yakilazimika kufungwa kutokana na kuchakaa na kuhatarisha usalama wa wanafunzi.

KAULI YA DC

Alipotafutwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka, alisema kuwa wilaya yake bado inahitaji kupata misaada ya wadau ili kuweza kusukuma maendeleo katika jimbo hilo na hajawahi kuzuia misaada ya wadau.

DC Chikoka, alisema kuwa Mkoa wa Mara uliweka utaratibu wa kupokea misaada katika ngazi mbalimbali ikiwamo wilaya, ambapo wadau hutakiwa kuandika barua ya nia yao au hata kuombwa na hupokelewa na ofisi yake kisha naye hukabidhi kwa Mkurugenzi ili kuipeleka kwenye maeneo yenye mahitaji zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka.

“Kwanza nikushukuru siwezi kuzuia misaada na haitokea kufanya hivyo, ila hao wanaotoa misaada wapo ambao wana nia ya kutaka ubunge utaratibu wetu ni kwamba tayari hapa yupo Mbunge (Jaffari Chege) anatakiwa kupewa ushirikiano.

“Na leo ukiruhusu kila ambaye ana msaada wake kwa kipindi hiki apite kwenye maeneo ya kata na vijiji si itakuwa vurugu, hawa wapeleke madawati ambayo tayari nimeshayapokea lakini wao walitaka tena waanze kupelekea.

“Utaratibu ukishapokea misaada hasa kama mimi DC ninatakiwa kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye yeye anajua zaidi ni eneo gani lenye mahitaji kwa wakati huu,” alisema DC Chikoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles