29.7 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

DAWA KINGA YA UKIMWI YAZINDULIWA

Na ELIUD NGONDO- MBEYA


 

SERIKALI imeanza majaribio ya dawa ya kuzuia Virusi Vya Ukimwi (HIV) inayojulikana kwa jina la Truvada.

Hata hivyo jamii imetakiwa kutambua kuwa hiyo si dawa ya kuzuia Ukimwi na watumiaji wametakiwa kuendelea kuchukua hadhari za kujikinga na ugonjwa huo.

Uzinduzi wa dawa hiyo ulifanyika juzi jijini Mbeya ambapo kwa awamu ya kwanza dawa hizo zitasambazwa katika mikoa 14 ya majaribio.

Akizungumza na MTANZANIA jana Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alisema kuzinduliwa kwa dawa hiyo mahsusi kutamsaidia mtu asiweze kupata maambukizi.

“Jana (juzi) kulikuwa na taarifa kwamba Tanzania tumezindua tiba au kinga dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, taarifa hiyo si sahihi, hatujapata tiba mpaka sasa hivi.

“Kinachoendelea tumezindua dawa kinga lengo ni kwamba tunataka tuielekeze katika makundi ambayo tunayaona yapo katika hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa huu,” alisema Dk. Ndugulile

Alisema makundi hayo yanapatiwa dawa hii kwa lengo la kuwakinga wasipate Virusi Vya Ukimwi lakini dawa hiyo si suluhisho la kuacha kutumia kinga nyingine za kawaida.

“Hatujapata tiba ya virusi vya ukimwi na utaratibu huu tunaanza majaribio hivi sasa. Leo hii tunatafakari mpango mkakati wa nne na tuna wa miaka 30, tumetoka wapi, tupo wapi na tunaenda wapi, tunajua jinsi unavyoambukizwa tuna malengo ya kinchi na yapo malengo ya kidunia bado tuna changamoto nyingi hasa za kuyapata na kuyaingiza makundi mbalimbali kwenye dawa,” alisema.

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles