27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

Davido asaini mkataba RCA Records

David Adeleke ‘Davido’
David Adeleke ‘Davido’

NEW YORK, MAREKANI

MKALI wa muziki kutoka nchini Nigeria, David Adeleke ‘Davido’, amefanikiwa kusaini mkataba na kampuni ya muziki ya RCA Records, ikiwa mapema mwaka huu alisaini mkataba na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

RCA Record ni rekodi ya muziki nchini Marekani, ambayo inasimamia kazi za wasanii wa muziki aina ya pop, rock, hip-hop, RnB, blues na jazz, na sasa inasimamia kazi za wasanii wakubwa kama vile ASAP Ferg, ASAP Rocky, Alicia Keys, Aretha Franklin, Zayn Malik, Usher Raymond, T-Pain, Shakira, Justin Timberlake, Pink na wengine wengi.

Mbali na Davido, lebo hiyo imeweza kusainisha msanii mwingine kutoka nchini Nigeria, Ayo Jay, mapema mwaka huu.

“Nina furaha kubwa kusainiwa na kampuni kubwa kama hiyo, hivyo kazi zangu zitakuwa bora zaidi, kuna wasanii wakubwa ambao natakiwa kufanya nao kazi hivi karibuni kama vile Tinashe, Trey Songz na Young Thug,” aliandika Davido.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles