Kim Kardashian asumbuliwa na meno

Kim Kardashian
Kim Kardashian
Kim Kardashian

NEW YORK, MAREKANI

MKE wa rapa Kanye West, Kim Kardashian, inadaiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa meno, hivyo anashindwa kutafuna vitu vigumu.

Mrembo huyo aligundua hilo juzi jijini New York, na kujikuta akishindwa kula chakula kutokana na maumivu makali kwenye meno.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo aliweka wazi kupatwa na tatizo hilo, lakini iliweza kuwasiliana na daktari wake kwa ajili ya matibabu.

“Nilipatwa na maumivu ya ghafla nikawa nashindwa kutafuna kitu chochote chenye ugumu, lakini niliwasiliana na daktari wangu kisha nikafanyiwa matibabu, kwa sasa naendelea vizuri na chakula kinaliwa kama kawaida,” aliandika Kim Kardashian.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here