28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Daladala za muda kutoa huduma kukabili corona

Na Mwandishi Wetu –Dar es Salaam 

ZIKIWA ni siku chache tangu daladala zipigwe marufuku kusimamisha abiria, ikiwa ni njia ya kukabiliana na corona, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) imetoa wito kwa watu binafsi, shule na taasisi zenye mabasi ambayo hayajapangiwa njia kuomba leseni za muda mfupi ili watoe huduma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Gilliad Ngewe, watu wenye mabasi ya abiria ambao hawajapangiwa njia wametakiwa kufika ofisi za mamlaka hiyo kuomba leseni kusudi kuanza kutoa huduma hiyo.

Hivi karibuni Latra iliagiza mabasi yote yaendayo haraka (BRT) na daladala zote  kubeba abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo, ukiwa ni mkakati wa kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona (Covud-19).

Pia Latra iliagiza kila chombo cha usafiri kiwe na dawa ya kuua virusi mikononi (hand sanitizer) kabla ya abiria kuingia ndani ya basi asafishe mikono kwa dawa ya kuua virusi mikononi.

Ngewe alisema utekelezaji wa agizo hilo ni hatua ya kujikinga dhidi ya virusi vya corona katika vyombo vya usafiri.

” Latra imekutana na wadau wa usafiri na usafirishaji ardhini na kutafakari kuweka mikakati ya kukabiliana na janga hili, wamiliki wote na wafanyakazi wao wanaagizwa kuhakikisha wananyunyizia mabasi yao dawa kila mwisho wa safari.

“Pia Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (Tazara) wahakikishe treni zinapulizwa dawa kila mwisho wa safari,” alisema Ngewe.

Mbali na hilo, Ngewe alisema kwa magari ya mizigo hayaruhusiwi kubeba abiria yeyote huku akisisitiza elimu juu ya kujikinga na virusi vya corona itolewe ndani ya vyombo vya usafiri kwa kutumia redio na runinga katika magari hayo.

“Lakini hatua nyingine, kuanzia sasa haitoruhusiwa watu wanaomsindikiza abiria kuingia katika vituo vya treni au mabasi yaendeyo mikoani,” alisema Ngewe.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles