24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 25, 2022

CWT yahimiza hatua stahiki mwalimu aliyecharazwa bakora

Na IBRAHIM YASSIN, KATAVI

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Katavi, kimeziomba Mamlaka zinazohusika ziingilie katika kwa kitendo cha mwalimu wa Shule ya Msingi Usevya iliyopo Katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele, Jiyabo Ng’wanzalima kuchapwa viboko  na Ofisa Elimu Kata, Mwalimu Daniel Mlumuka kwa madai ya kutohudhuria shuleni au kazini.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Katavi, Jumanne Msomba aliwaambia waandishi wa habari mjini Mpanda jana na kulaani kitendo hicho, akisisitiza kuwa kimeidharirirsha tasnia ya walimu,na kuomba hatua ziweze kuchukuliwa dhidi ya ofisa elimu huyo.

Inadaiwa Mwalimu Ng’wanzalima wa Shule ya Msingi ya Usevya hakuhudhuria kazini siku moja, na baadae Ofisa Elimu Kata,  mwalimu Mlimuka alimfuata nyumbani kwake akiwa ameongoza na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Usevya, Geofrey Sikale na kudaiwa kumcharaza viboko mwalimu huyo kwa kutokufika kazini kwake.

Msomba, Mwenyekiti wa CWT Katavi akieleza masikitiko na kulaani kitendo cha mwalimu kuchapwa viboko na Ofisa elimu huyo akisema kitendo hicho ni cha kwanza kutokea mkoani Katavi.

Alisema suala hilo ni la udhalilishaji na kwamba anaziomba mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya afisa huyo kwani kitendo alichofanyiwa mwallimu mwenzao kinarudisha morali ya walimu kufanya kazi.

Katibu wa CWT mkoani Katavi, Rosemery Mwakibete alisema wao kama viongozi wanalaani kitendo hicho huku wakitaka ofisa huyo awajibishwe na mamlaka husika kutokana na kitendo cha udhalilishaji alichokifanya kwani kitendo cha mwalimu kuchapwa viboko hakikubaliki.

“Sisi ni walimu, tunafanya kazi katika mazingira magumu na pia huwa tunachukua muda wetu kuhakikisha tunawafundisha wanafunzi ili waweze kufanya vizuri darasani, sasa kitenda alichokifanya ofisa huyo kinarudisha moyo kwa walimu kujituma ,tunaomba mamlaka husika zichukue hatua dhidi yake,” alisema.

Imeelezwa kuwa mwalimu huyo wa Shule ya Msingi Usevya iliyopo halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele, Ng’wanzalima alichapwa viboko kadhaa akiwa kazini na ofisa elimu kwa madai kuwa hahudhurii darasani kufundisha, kitendo ambacho kimechukuliwa kama ni uudhalilishaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,160FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles